POST: AFISA USIMAMIZI NYANDA ZA MALISHO II (RANGE MANAGEMENT OFFICER II) - 4 POST
EMPLOYER: Wizara ya Mifugo na Uvuvi-UVUVI -Mifugo
APPLICATION TIMELINE:: 2024-12-07 2024-12-17
JOB SUMMARY: NA
DUTIES AND RESPONSIBILITIES:
- Kubuni mbinu na miradi ya uendelezaji malisho na maji ya mifugo wilayani na kusimamia utekelezaji wake
- Kuratibu mipango ya ugani ya uendelezaji wa malisho
- Kufanya mafunzo ya uendelezaji malisho na vyanzo vya maji ya mifugo, kwa wataalam na wafugaji na wadau wengine
- Kufanya tafiti za rasilimali (Range resources survey) ya mifugo, vyakula vya mifugo, malisho na vyanzo vya maji
- Kusimamia na kudhibiti uharibifu wa mazingira katika maeneo ya nyanda za malisho katika wilaya
- Kushiriki katika shughuli za kudhibiti uvamizi wa maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya ufugaji na njia za mifugo wilayani
- Kufuatilia, kuweka, kuchambua na kutafsiri takwimu za uendelezaji, matumizi na uhifadhi wa malisho wilayani
- Kufanya uchunguzi wa kina kuchora ramani za usambaaji wa mbung'o na ndorobo katika maeneo yao
- Kuhamasisha wananchi kushiriki katika njia/ mbinu bora na rahisi za kuzuia ndorobo. x.Kutayarisha taarifa za robo, nusu na mwaka za uzuiaji wa mbung'o, Ndorobo, nagana, malale na hali ya malisho
- Kufanya kazi nyingine zozote za fani yake atakazoagizwa na kupangiwa na Mkuu wake
QUALIFICATION AND EXPERIENCE:
Kuajiriwa wenye Shahada ya Kwanza katika mojawapo ya fani ya Usimamizi wa Nyanda za Malisho (Range Management), Usimamizi wa Maliasili au Usimamizi wa Maeneo Kame kutoka chuo Kikuu cha Sokoine au sifa inayolingana na hiyo kutoka chuo kingine kinachotambulika na Serikali.
REMUNERATION: TGS D