POST: AFISA MAENDELEO YA JAMII DARAJA II (COMMUNITY DEVELOPMENT OFFICER GRADE II) - 5 POST
EMPLOYER: MDAs & LGAs
APPLICATION TIMELINE:: 2025-01-07 2025-01-20
JOB SUMMARY: NA
DUTIES AND RESPONSIBILITIES:
- i.Kuandaa na kupendekeza mipango na mikakakati ya kubadili fikra za watu ili waweze kuwa na mawazo ya maendeleo sawia na Sera za Serikali na wakati uliopo
- Kupitia mbinu shirikishi kuwezesha jamii kuanzisha miradi ya kijamii
- Kuhamasisha matumizi endelevu ya mazingira
- Kusambaza na kuhamasisha matumizi ya teknolojia sahihi kama vile uvunaji wa maji ya mvua, majiko sanifu, matumizi ya mikokoteni
- Kuhamasisha watu kutumia huduma za mafunzo ya Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi
- Kuwasadia wanachi vijijini kuandaa maandiko (Project Write ups) ya kuombea fedha za kuendesha miradi yao
- Kuhamasisha, kuandaa na kutoa elimu kwa umma kuhusu uraia na Utawala bora
- Kukusanya, kutunza, kutafsiri na kusambaza takwimu na kumbukumbu muhimu kwa ajili ya matumizi ya jamii
- Kuwezesha wananchi kupambana na mila zenye madhara kwa afya za wanchi hasa wanawake na watoto wa kike, kuenea kwa virusi vya UKIMWI na magonjwa ya mlipuk
- Kuelimisha viongozi wa Serikali za Vijiji, Dini na Mashirika yasiyo ya Kiserikali kuhusu Sera mbalimbali za Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto na kutumia Sera hizo
- na xi.Kutoa taarifa za hali ya jamii kwa ngazi mbalimbali.
QUALIFICATION AND EXPERIENCE:
Kuajiriwa wahitimu wa Shahada au Stashahada ya Juu ya Maendeleo ya Jamii kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali waliojiimarisha katika moja ya fani zifuatazo:- Maendeleo ya Jamii (Community Development), Elimu ya Jamii (Sociology), Masomo ya Maendeleo (Development Studies), Mipango na Usimamizi wa Miradi na Menejimenti (Project Planning and Management) au Jinsia na Maendeleo (Gender and Development).
REMUNERATION: TGS.D