POST: AFISA USIMAMIZI NYANDA ZA MALISHO MSAIDIZI DARAJA LA II (RANGE MANAGEMENT FIELD OFFICER II) - 4 POST
EMPLOYER: Wizara ya Mifugo na Uvuvi-UVUVI -Mifugo
APPLICATION TIMELINE:: 2024-12-07 2024-12-17
JOB SUMMARY: NA
DUTIES AND RESPONSIBILITIES:
- Kufanya na kusimamia uchunguzi wa hali ya nyanda za malisho (trend), mbung'o na ndorobo katika eneo lake
- ii.Kushirikiana na wahudumu wa nyanda za malisho kutembelea wafugaji na kuwapa ushauri fasaha wa kitaalam kuhusu uzalishaji na uhifadhi wa malisho katika eneo lake la kazi
- Kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya nyanda za malisho, vyakula vya ziada, maji ya mifugo na mbinu za uzuiaji wa mbung'o na ndorobo kwa wafugaji
- Kushauri na kuwaelekeza wafugaji na wadau wengine kuzalisha malisho na kuhifadhi malisho kwa kutumia njia mbalimbali kama hei/saileji/kutengwa yakiwa shambani bila kuchungwa
- Kukusanya na kutunza takwimu za malisho, mbung'o na ndorobo
- Kutayarisha ramani za usambaaji wa mbung'o na ndorobo katika eneo lake
- Kupanga na kusimamia shughuli zote za uzuiaji mbung'o na ndorobo katika eneo lake
- Kuhamasisha utumiaji wa mbinu salama za uzuiaji wa mbung'o na ndorobo kwa kuzingatia kanuni ya hifadhi ya mazingira
- Kufuatilia taarifa za awali za kuwepo kwa matukio ya ndorobo (nagana na malale). x.Kuandaa taarifa za robo, nusu na mwaka za hali ya malisho na uzuiaji wa mbung'o na ndorobo
- na xi.Kufanya kazi nyingine zozote za fani yake itakavyoelekezwa na mkuu wake wa kazi.
QUALIFICATION AND EXPERIENCE:
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV au VI wenye Stashahada (Diploma-NTA Level 6) katika Nyanda za Malisho na Udhibiti wa Ndorobo kutoka Vyuo vya Wakala wa Mafunzo ya Mifugo (Livestock Training Agency - LITA) au sifa inayolingana na hiyo kutoka vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.
REMUNERATION: TGS B