POST: MLEZI WA WATOTO MSAIDIZI (CHILD CARE ASSISTANT) - 1 POST
EMPLOYER: Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi
APPLICATION TIMELINE:: 2024-11-08 2024-11-21
JOB SUMMARY: NA
DUTIES AND RESPONSIBILITIES:
- Kushiriki kutekeleza mpango jumui wa Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya watoto, (ECD integrated plan)
- Kuandaa na kutekeleza ratiba ya shughuli za kila siku katika kituo husika
- Kubainisha na kutumia mazingira salama ya kujifunzia watoto
- Kutoa rufaa ya masuala ya watoto yaliyo nje ya uwezo wake
- Kutambua watoto wenye mahitaji maalumu na kutoa huduma stahiki
- Kushiriki katika uhamasishaji wa jamii katika kutoa huduma za malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto
- Kutoa ushauri kwa wazazi/walezi kuhusu malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya watoto katika eneo lake
- Kuandaa na kutoa taarifa ya utekelezaji wa shughuli za kila siku katika eneo husika
- Kushiriki kwenye mchakato wa uendeshaji wa mashauri ya watoto katika ngazi husika (case management)
- Kuandaa taarifa ya uanzishaji wa vituo vya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto katika maeneo husika
- na xi.Kufanya kazi nyingine yoyote atakayopangiwa na Mkuu wake wa kazi kulingana na elimu na ujuzi wake.
QUALIFICATION AND EXPERIENCE:
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne au kidato cha sita waliohitimu mafunzo ya Astashahada katika mojawapo ya fani zifuatazo:- Elimu ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto, Ustawi wa Jamii, Saikolojia kutoka Chuo kinachotambulika na Serikali.
REMUNERATION: TGS B